Vikongwe kuhudhuria swalah ya ijumaa

Swali: Je, inajuzu kwa wanawake watuwazima kuswali swalah ya ijumaa?

Jibu: Ndio, inajuzu kwao. Kwa sharti watoke kwa njia ya Kishari´ah. Kwa msemo mwingine wasiwe ni wenye kujitia manukato wala wenye kujishaua kwa kuonyesha mapambo. Wawe sehemu ya kipekee wenye kujitenga na wanaume au mbali na wao kwa njia ya kwamba hawatochanganyikana na wanaume. Kadhalika punde tu baada ya imamu kutoa salamu waharakishe kusimama kutoka nje ili watoke kabla ya wanaume na kabla ya kusongamana nao. Wakiswali pamoja na imamu wa ijumaa ni sahihi na ule uwajibu wa kuswali Dhuhr umedodonka kwao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (09) http://binothaimeen.net/content/6729
  • Imechapishwa: 13/11/2020