Vijana warejee kwa wanachuoni na wasiweki maji juu ya vichwa vyao

Swali: Ni zipi nasaha zako juu ya ndugu zetu Misri khaswa kwa kuzingatia hali uliyoitaja?

Jibu: Nasaha zangu daima ni kusafisha na kulea, Tasfiyah wa Tarbiyah. Kwa msemo mwingine mafunzo…

Muulizaji: Je, unaweza kuwapa kalima inayowahusu wao peke yao juu ya mada hii ya Takfiyr?

Jibu: Nafikiria kuwa watu hawa hawawezi kunasihiwa mpaka kwanza watambue nafasi ya nafsi zao. Asiweko yeyote katika wao ambaye atafikiria kuwa ana elimu au ana kitu ilihali ukweli wa mambo ni kwamba hawana chochote. Nawanasihi wawasiliane na wale wanachuoni wanaowaamini ambao, pamoja nao, wanarejea katika Qur-aan na Sunnah kisha wanatofautiana nao inapokuja katika kurejea katika mfumo wa Salaf. Nawanasihi wote kujenga dhana mbaya juu ya elimu yao kwanza na wajenge dhana nzuri juu ya wanachuoni wao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakutoacha kuwepo kikundi katika Ummah wangu chenye kushinda juu ya haki. Hawatodhurika na wale wenye kuwakosesha nusura mpaka itapokuja amri ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) na wao bado wako juu ya hayo.”

Ni lazima katika ulimwengu wa Kiislamu wawepo wanachuoni ambao watu wanarudi kwao. Hawawezi kuwa vijana hawa ambao dogo linaloweza kusemwa juu yao ni kwamba wameghurika juu ya elimu yao kwamba eti ndio lile kundi ambalo ameliashiria Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth hii Swahiyh na khaswa ukizingatia kwamba zipo Hadiyth Swahiyh zinazoashiria baadhi ya maeneo yenye sifa ya kipekee kwa elimu au imani. Hadiyth iliyotajwa punde imepokelewa na al-Bukhaariy katika ”as-Swahiyh” yake kupitia kwa Mu´aawiyah bin Abiy Sufyaan (Radhiya Allaahu ´anh). Siku moja aliwakhutubia watu ambapo akataja Hadiyth hii kisha akasema:

”Mu´aadh huyu hapa anasema kwamba wanapatikana Shaam.”

Hadiyth hii inaashiria kwamba elimu itakuweko zaidi katika miji ya Kiislamu kuliko ilivyo katika miji mingine. Ipo Hadiyth nyingine inayosema:

”Imani itakusanyika al-Madiynah kama ambavo nyoka inavyojikusanya shimoni mwake.”[1]

Nawanasihi vijana hawa, na wengineo katika miji mbalimbali ya Kiislamu, ambao bado ndio wako mwanzoni kabisa katika mambo ya elimu wasiyaweki maji juu ya vichwa vyao, wasidanganyike kwa elimu yao nyonge na waulize kama alivosema Mola wa walimwengu:

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Hivyo basi waulizeni watu wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.”[2]

[1] al-Bukhaariy (1777).

[2] 16:43

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (1012)
  • Imechapishwa: 07/11/2020