Swali: Swali lako linahusiana na mtu ambaye anasumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa takriban muda wa miaka minane sasa na kwamba bado yuko katika matibabu. Madaktari wamefanya uchunguzi mara kadhaa na wakaona kuwa anasumbuliwa na maradhi hayo. Wamemshauri kutofunga kwa sababu ya kuepuka maradhi yasiongezeke na hali kuwa mbaya zaidi. Vilevile wamesema kuwa akifunga, basi maradhi yatamkwamisha na hawezi kuendelea. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Baada ya kuliangalia suala lake, tunaona kuwa analazimika kula. Baada ya hapo atalazimika kulipa masiku yake baada ya kupona kwake ikiwa ndio linalotarajiwa. Mambo yasipokuwa hivo na asiponye kutokana na maradhi, basi atamlisha chakula masikini kwa kila siku moja iliyompita.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/180)
  • Imechapishwa: 21/03/2024