Swali: Je, ni Sunnah kuvaa pete ya fedha kwenye kidole cha pete au kwenye kidole kidogo?

Jibu: Kwa hali yoyote. Ni sawa kuvaa pete kwenye vyote viwili. Lakini je, ni ni Sunnah? Wanazuoni wametofautiana juu ya suala hilo. Wako wanaosema kuwa ni Sunnah kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alivaa pete. Maswahaba pia walifanya hivo. Kwa sharti pete hiyo isiwe ni ya dhahabu.

Wengine wakasema kuwa pete ni Sunnah tu kwa watu wenye mamlaka kama vile wenye watawala, mahakimu na wenye kutoa fatwa. Kwa jumla ni kwamba hakika si Sunnah kuvaa pete, lakini haijakatazwa pia.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/161)
  • Imechapishwa: 15/05/2026