Swali: Kipindi cha mwisho kumejitokeza viatu ambavyo vinafanana na viatu vya wanaume upande wa vidole? Ni ipi hukumu ya kuvivaa?

Jibu: Naona kuwa kuvivaa ni haramu. Kwa sababu nimeona uinje wake ni viatu vya wanaume na mtu hawezi kutilia shaka yoyote kuwa ni viatu vya wanaume. Ni kweli kwamba chini yake kwenye kisigino sio kama viatu vya wanaume. Lakini hukumu imefungamana na ule uinje. Lakini uinje pindi mtu atakapoviona atahukumu kuwa ni viatu vya wanaume. Sifa zake zote ni kama viatu vya wanaume. Kuvaa viatu kama hivi ni haramu. Kuviuza ni haramu. Kuvinunua ni haramu. Baya zaidi kuliko yote haya ni kwamba:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kujifananisha na wanaume na amewalaani wanaume wenye kujifananisha na wanawake.”

Je, hivi kweli kuna yeyote ambaye anaridhia kuingia ndani ya laana za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Hakuna yeyote anayeridhia haya. Kwa sababu hiyo napendekeza kususiwa kwa viatu hivi na visiuzwe. Ninamuomba Allaah awaamshe wale wahusika juu ya vile vinavyoingizwa ndani ya nchi hii katika mfano wa mambo kama haya ili waweze kuzuia vile ambavyo ni haramu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (65) http://binothaimeen.net/content/1462
  • Imechapishwa: 09/08/2020