Uwajibu wa kuitikia salamu

Swali: Vipi hukumu ya kuitikia salamu?

Jibu: Ni wajibu. Hilo ni tofauti na kuanza; ni wajibu au sio wajibu? Kuhusu kuitikia ni wajibu, kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا

“Mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo.” (04:86)

Bora ni kuitikia kwa kilicho bora zaidi. Hata hivyo ni wajibu kuitikia.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23940/ما-حكم-رد-السلام
  • Imechapishwa: 02/08/2024