98. Uwajibu wa kuamini ´Aqiydah hii katika maisha yako yote

Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

إِذَا مَا اعْتقدْت الدهْرَ يا صَاحِ هذهِ

40 – Midhali utaendelea daima kuyaitakidi haya, ee rafiki yangu

فأَنْت عَلَى خَيْرٍ تبيتُ وتُصْبِحُ

     basi wewe utakuwa katika kheri jioni na asubuhi

MAELEZO

Hii ni hitimisho. Ukiendelea kuyaamini yale yote yaliyomo kwenye shairi hili katika uhai wako wote na mwisho wa uhai wako, basi wewe uko katika kheri duniani na Aakhirah. Ama ukiyaamini kwa kipindi fulani halafu ukayaacha na kuyapuuza, hayatokufaa kitu. Ni lazima uendelee kuamini ´Aqiydah hii katika maisha yako yote mpaka pale utapokufa. Kuhusu yule ambaye atayaamini mara ya kwanza kisha akajireje kwayo, huyu ataangamia pamoja na wenye kuangamia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 202
  • Imechapishwa: 13/01/2024