Swali: Ulisema katika darsa iliyopita kuwa kundi la al-Ikhwaan al-Muslimuun na Jamaa´at-ut-Tabliygh si katika makafiri, bali ni katika Ahl-ul-Bid´ah; je ni katika makundi mapotofu yatayoangamia kama ilivyokuja katika Hadiyth ya mgawanyiko?

Jibu: Sikumbuki kama nilisema kauli hii, ila maana yake ni sahihi. Si makafiri – Allaah akitaka. Lakini wako na mikhalafa kutokana na mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Da´wah, wako na mukhaalafaat.

Ni wajibu kwao kusahihisha makosa yao na wawe katika mfumo sahihi – mfumo wa Da´wah na walinganie katika Tawhiyd na wakataze shirki. Huu ndo wajibu.

Lakini hatujawahi kusikia wakikataza shirki, na wala hatujawahi kusikia wakilingania katika Tawhiyd. Huu ni upungufu mkubwa na Da´wah haiwezi kuwa sahihi kwa mfumo huu.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127630
  • Imechapishwa: 03/09/2020