Swali: Nilichukua mkopo kutoka benki ya ardhi juu ya kiwanja changu, kisha baada ya kupokea malipo ya kwanza ya 30,000 alikuja mtu akanipa 20,000 pamoja na zile 30,000, nikamuuzia kiwanja. Lakini mkopo bado uko kwa jina langu, naye ndiye anaishi humo na hakulipa benki ilihali makubaliano yalikuwa yeye atalipa. Nipe fatwa mimi na wengine wanaofanya njia hii?
Jibu: Tunachojua ni kuwa ardhi hiyo imewekwa rehani kwa benki na haiwezi kuuzwa. Wala benki hairuhusu iuzwe isipokuwa kwa idhini yake au kwa kulipwa deni lililoko juu ya mmiliki wake. Mwenye rehani ana haki ya kuzuia uuzaji. Mmiliki wa mali iliyowekwa rehani hana haki ya kuitumia au kuiuza mpaka apate ruhusa ya yule aliyeshikilia rehani. Kwa hiyo mali hii iko chini ya rehani. Kwa hiyo ni lazima akubaliane na benki kuhusu jambo hili. Ikiwa benki itaruhusu kuuza kwa mtu fulani au mtu huyo kuchukua nafasi yake katika mkopo, basi hakuna ubaya katika hilo. Ikiwa pia mamlaka imeruhusu na kutoa ruhusa kwa watu kufanya hivyo, basi hapana tatizo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3209/حكم-بيع-الرهن-من-قبل-الراهن
- Imechapishwa: 02/08/2026
Swali: Nilichukua mkopo kutoka benki ya ardhi juu ya kiwanja changu, kisha baada ya kupokea malipo ya kwanza ya 30,000 alikuja mtu akanipa 20,000 pamoja na zile 30,000, nikamuuzia kiwanja. Lakini mkopo bado uko kwa jina langu, naye ndiye anaishi humo na hakulipa benki ilihali makubaliano yalikuwa yeye atalipa. Nipe fatwa mimi na wengine wanaofanya njia hii?
Jibu: Tunachojua ni kuwa ardhi hiyo imewekwa rehani kwa benki na haiwezi kuuzwa. Wala benki hairuhusu iuzwe isipokuwa kwa idhini yake au kwa kulipwa deni lililoko juu ya mmiliki wake. Mwenye rehani ana haki ya kuzuia uuzaji. Mmiliki wa mali iliyowekwa rehani hana haki ya kuitumia au kuiuza mpaka apate ruhusa ya yule aliyeshikilia rehani. Kwa hiyo mali hii iko chini ya rehani. Kwa hiyo ni lazima akubaliane na benki kuhusu jambo hili. Ikiwa benki itaruhusu kuuza kwa mtu fulani au mtu huyo kuchukua nafasi yake katika mkopo, basi hakuna ubaya katika hilo. Ikiwa pia mamlaka imeruhusu na kutoa ruhusa kwa watu kufanya hivyo, basi hapana tatizo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3209/حكم-بيع-الرهن-من-قبل-الراهن
Imechapishwa: 02/08/2026
https://firqatunnajia.com/uuzaji-wa-mali-iliyowekewa-rehani-na-mkopeshaji/