Hapana vibaya kuwasalimia wanawake

Swali: Je, inajuzu mtu akipita kwa wanawake awasalimie?

Jibu: Ndiyo, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwasalimia wanawake, aliwapa salamu na pia aliashiria kwa mkono, kama mlivyosikia katika semina. Hivyo akiwapa salamu kwa kusema:

السلام عليكم

“Amani iwe juu yenu.”

Nao wakajbu:

وعليكم السلام

“Nanyi amani iwe juu yenu.”

Ikiwa wako mbali, ataashiria kwa mkono na atoe salamu ili waelewe. Vivyo hivyo kwa wanaume wengine ikiwa wako mbali au katika sehemu ambayo anaogopa hawatasikia, basi atatoa salamu na ataashiria.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3208/حكم-القاء-السلام-على-النساء
  • Imechapishwa: 02/08/2026