Usuguaji wa viungo wakati wa kutawadha na josho

Swali: Je, kusugua viungo wakati wa josho na wudhuu´ ni lazima?

Jibu: Ndio, kusugua ni jambo linalopendekezwa, si wajibu. Imepokelewa katika baadhi ya Hadiyth kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisugua mikono yake hadi kwenye viwiko. Kwa hivyo hakuna tatizo kama mtu atasugua kwa nia ya kufanya jambo linalopendekezwa. Lakini kwa upande mwingi wa vitendo vya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusugua, bali alikuwa akipitisha maji tu. Kwa kuwa hiyo ni nyepesi zaidi kwa waislamu. Kwa hivyo kupitisha maji kunatosha. Ikiwa kutakuwa na haja ya kusugua, hakuna tatizo.

Swali: Hivyo pia katika josho?

Jibu: Ndio, katika josho vivyo hivyo. Ikiwa maji yatapita juu ya mwili wote yanatosha. Lakini kama kutakuwa na sehemu zenye vitu kama udongo, unga au vitu vingine vinavyozuia maji, basi sehemu hizo zasuguliwa hadi vitu hivyo viondoke.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31514/ما-حكم-الدلك-في-الغسل-والوضوء
  • Imechapishwa: 30/10/2025