Kuufungamanisha moyo na viumbe ni jambo lenye kulaumika. Linalotakikana ni mtu kuufungamanisha moyo wake na Allaah na amtegemee Allaah. Aufungamanishe moyo wake kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) na asiufungamanishe moyo wake kwa viumbe hata kama watakuwa ni sababu. Awatazame kwa njia ya kwamba wao ni sababu [tu]. Mnufaishaji na ambaye hufanya sababu kutokea na kunuifaisha nayo, ni Allaah (Jalla wa ´Alaa). Jambo hili likipatikana ndani ya moyo, basi mja huwa pamoja na Mola Wake (´Azza wa Jall) na hutambua kuwa hakukuwi jambo isipokuwa yale aliyomkadiria na kumwandikia Allaah (Jalla wa ´Alaa).
- Muhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 286
- Imechapishwa: 14/05/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)