Muulizaji: Wakati imamu ´Aliy alipokuwa anajibia swali alikuwa akitumia neno “Qaaluun”, lililo na maana ya “vizuri” kwa kirumi…
al-Albaaniy: Usisemi kwa mara nyingine tena “imamu ´Aliy”.
Muulizaji: Si alikuwa ni imamu.
al-Albaaniy: Abu Bakr naye?
Muulizaji: Imamu.
al-Albaaniy: Ulishawahi siku moja wapo kusema “imamu Abu Bakr?” Sema hapana.
Muulizaji: Hapana.
al-Albaaniy: Kwa hiyo nitakwambia kitu baina yako wewe na mimi asiweko yeyote atakayetusikia: huo ni mwenendo wa kitu kilichofichwa.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (1023)
- Imechapishwa: 02/10/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related

al-Albaaniy ni Mujtahid
https://www.youtube.com/watch?v=4HW0kd2OWQM Swali: Nimesikiliza moja ya kaseti ya Imaam Muhammad Naaswiyrud-Diyn al-Albaaniy katika masuala anaposema imamu "Aamiyn" nanyi semeni "Aamiyn". Akakazia hilo. Ibn ´Uthaymiyn: Kasema nini? Muulizaji: Kasema ni wajibu anaposema imamu "Aamiyn" kusema baada yake "Aamiyn" na kwamba uliyoyasema ni kosa. Ibn Ibn ´Uthaymiyn: Umemsikia kweli kasema hivyo? Muulizaji: Ndiyo.…
In "Utetezi kwa al-Albaaniy"
5. Shari´ah ya wanawake kuswali mkusanyiko
[6] Imewekwa katika Shari´ah kwa wanawake kuhudhuria swalah hizi kujengea Hadiyth ya Abu Dharr iliyotangulia. Bali inafaa kuwateulia imamu ambaye atakuwa ni wa kwao peke yao mbali na yule imamu wa wanaume. Imethibiti kuwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) pindi alipowakusanya watu juu ya swalah za nyusiku, alimteua Ubayy bin Ka´b…
In "Qiyaam Ramadhwaan - al-Albaaniy"
Kuswali ´Ishaa nyuma ya anayeswali Tarawiyh II
Inajuzu kwa mtu kuswali swalah ya faradhi nyuma ya ambaye anaswali swalah ya Sunnah. Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema kwamba mtu ambaye amepitwa na swalah ya ´Ishaa na akaiswali nyuma ya anayeswali Tarawiyh, hakuna neno. Kujengea juu ya haya tunasema kitendo hichi ambacho hufanywa na baadhi ya watu…
In "Mkusanyiko (Jamaa´ah)"