Usiseme uwongo kwa ajili ya kuwachekesha watu

Swali: Ikiwa mtu yuko katika kundi kisha akamzungumzia mmoja wao kwa kusema jambo lisilo sahihi kwa lengo la kuwachekesha watu na mtu huyo aliyesemwa hakuridhia hilo. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Hairuhusiwi kwake kusema jambo litakalomuumiza mmoja wa waliopo, liwe ni uongo au liwe ni jambo linalomghadhabisha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hata kama anataka kuwachekesha watu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ole wake yule anayesimulia na kusema uongo ili awachekeshe watu! Ole wake, kisha ole wake!”

Haijuzu kwa mtu kusema batili ili kuwachekesha watu. Anapaswa kuuhifadhi ulimi wake na asiseme jambo la kuwachekesha watu hali ya kuwa lenyewe halijuzu. Huenda likawa ni uongo, kumtukana mtu au kumfanyia mzaha wa kumdhalilisha, yote haya ni mambo maovu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3345/حكم-الكذب-على-شخص-لاضحاك-الناس
  • Imechapishwa: 14/08/2026