Swali: Leo hii imekuwa ni jambo lililosambaa sana kati ya wanafunzi, sembuse watu wa kawaida, khaswa hapa kwetu kila pale ambapo mtu anamwombea du´aa ndugu yake kwa mfano akasema ”Allaah atujaalie sisi na nyinyi – Allaah akitaka”. Je, jambo hilo linaingia katika makatazo pia[1]?

Jibu: Ndio, linaingia ndani ya makatazo. Haifai kusema hivo. Asiseme ”Allaah akitaka”. Hii ni du´aa inayotakikana ambayo mja anakuwa mwenye kuihitaji sana.

Swali: Baadhi ya watu husema ”Uliyasema kwa ajili ya kutafuta baraka”?

Jibu: Hapana. Haitakikani wakati wa kuomba du´aa kusema mfano wa hayo.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/44-mlango-kuhusu-kusema-akitaka-allaah-na-wewe/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24288/حكم-الاستثناء-والتعليق-في-الدعاء
  • Imechapishwa: 24/09/2024