Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

50 – Makadirio ni siri ya Allaah (Ta´ala) katika viumbe Wake. Hakuna Malaika aliye karibu wala Mtume aliyetumilizwa aliyemfanya kujua jambo hilo. Kuzama na kupekua jambo hilo kutampelekea katika kukoseshwa nusura, kunyimwa na kuchupa mipaka.

MAELEZO

Pengine – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – makusudio ya kuchupa mipaka huku ni pale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

”Wakati kunapotajwa makadirio, basi nyamazeni.”

Ni Hadiyth Swahiyh na iliyosimuliwa kutoka kwa kikosi cha Maswahabah. Nimeitaja katika ”Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah”[1].

[1] Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (34).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 24/09/2024