Swali: Hadiyth ya ´Aaishah inayosema kwamba wakati wa kabla ya alfajiri ulikuwa ukimkuta Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hali ya kuwa amelala.

Jibu: Hilo ni baadhi ya nyakati. Au kinachokusudiwa ni kwamba ilikuwa inaweza kumtokea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hali hiyo. Ni kama mfano wa Daawuud ambaye alikuwa akilala nusu ya usiku, akasimama kuswali theluthi yake na akalala sehemu yake ya sita. Wakati mwingine alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akilala zaidi ya hivo ili apate nguvu ya matendo ya mchana. Akilala (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mapema basi huamka mapema kusimama usiku. Kwa hivyo Hadiyth zilizokuja kijumla zinafasiriwa kwa zile Hadiyth zilizo wazi na zinazofasiri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24336/%D8%AA%D9%88%D8%AC%D9%8A%D9%87-%D9%85%D8%A7-%D8%AC%D8%A7%D8%A1-%D9%81%D9%8A-%D9%86%D9%88%D9%85%D9%87-%EF%B7%BA-%D9%88%D9%82%D8%AA-%D8%A7%D9%84%D8%B3%D8%AD%D8%B1
  • Imechapishwa: 30/09/2024