Usimbebe mtoto wakati wa swalah ukijua kuwa amefanya haja

Swali: Amembeba mtoto wake ambaye yuko na najisi na yeye analijua hilo, hata hivyo kuna kizuizi kati yake na yeye?

Jibu: Maoni ya karibu zaidi na usahihi – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba asimbebe hali ya kuwa anajua yuko na najisi. Asimbebe kwa kufanyia kazi msingi unaosema kwamba mswaliji habebi najisi. Hata hivyo ni sawa asipojua au akajua kuwa ni msafi. Katika hali hiyo ambebe. Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimbeba Umaamah kwa kujengea ya kwamba ni msafi au hakujua hali yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24818/حكم-حمل-الطفل-في-الصلاة-وعليه-نجاسة
  • Imechapishwa: 13/12/2024