Swali: Vipi mnataka kutibu familia na jamii wakati kila sehemu imeharibika, ni mamoja iwe ni shule, mitaani au vyombo vya khabari? Tunatarajia jibu linalotosheleza kuhusu hili.

Jibu: Haipaswi kukata tamaa, ndugu yangu. Haipaswi kukata tamaa Pambana na pateni bishara njema na wala msikate tamaa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ

“Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye kumcha na wale watendao wema.”[1]

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا

“Na yeyote yuleanayemcha Allaah, atamjaalia njia [ya kutoka katika matatizo].”[2]

Kwa hiyo jukumu lako ni kujitahidi, kutokukata tamaa, kuwa na subira na kupambana ili kufanikiwa – Allaah akitaka – hata ikiwa ni kwa sehemu kubwa au wengi.

[1] 16:128

[2] 65:02

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2420/عدم-الياس-في-محاربة-المنكرات
  • Imechapishwa: 09/01/2026