Swali: Ni ipi hukumu ya kushirikiana na wahalifu kwa hoja eti anajuana na watu wengi na kwa ajili hiyo sisi tunaweza kuwafikia watu hao wengi na kuwaathiri?

Jibu: Ikiwa ushirikiano huo ni kwa njia ya kuwanasihi, kuwaelekeza na kuwaongoza, hapana vibaya. Ama ikiwa ni kwa ajili ya kuongeza wingi wao… Ikiwa mawasiliano yako naye kunaongeza idadi yao, hili ni tatizo na haijuzu. Lengo zuri halihalalishi njia. Je, mtu huyo ni katika Ahl-ul-Bid´ah au yuko tu na makosa mepesi? Ikiwa ni makosa tu mepesi, basi anasihiwe nayo, lakini ikiwa ni katika Ahl-ul-Bid´ah na hakubali nasaha, akate mawasiliano naye.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://darulhadith.com/samarbete-med-oliktankande-for-att-na-ut/
  • Imechapishwa: 31/08/2023