Swali: Kunapatikana majarida machafu yaliyoenea mikononi mwa vijana ambayo yanatoa matangazo ya uvutaji sigara, kuweka zawadi za kushawishi na kubeba matangazo ya uovu na ufuska. Je, kuna njia ya kufunga mlango wa shari hii, kuzuia na uangalizi wa kweli zaidi ya ule wa sasa?

Jibu: Hili ni lazima. Vitu hivi vinapopatikana ni wajibu kwa waandishi kuandika na kukemea na kwa wanazuoni kufikisha. Yeyote atakayekuta jambo kama hili anapaswa kutoa taarifa pia, kwa sababu mwanazuoni au mwandishi huenda akaghafilika au jambo likampita. Basi yule anayeliona na akaona halijaandikwa wala halijakemewa, basi inafaa aandikie wanazuoni na awakumbushe hadi walikemee ili kuwepo ushirikiano kati ya mwanazuoni, mwanafunzi, watu mashuhuri miongoni mwa waislamu na kati yao na dola pia. Kwa hiyo ushirikiano ni wajibu kati ya dola, wanazuoni na watu mashuhuri wa Kiislamu kila mahali katika nchi hii na nchi nyingine. Haijuzu kabisa kunyamaza. Watu watakuwa katika kheri maadamu wanashirikiana, wanaandika na wananasihana. Ama wakinyamaza, huo ndio mlango wa shari na balaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1025/خطورة-المجلات-الخليعة-والواجب-نحوها
  • Imechapishwa: 09/01/2026