Swali: Tunakuuliza kuhusu wanaume wa dini ambao ni vijana hii leo ambao wameshikamana na dini wanapingana hawa kwa hawa katika mambo ya dini kwa njia ya kwamba unamkuta mmoja anamfuata Shaykh fulani na mwingine anamfuata Shaykh mwingine. Unasemaje juu ya hili?
Jibu: Maoni yangu kwa kifupi ni kwamba ushabiki hautakiwi kuwa isipokuwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu yeye pekee ndiye amekingwa na kukosea na hazungumzi kwa matamanio. Haitakiwi kwa wanafunzi kufanya ushabiki kwa watu – ni mamoja wamepatia au wamekosea. Kwa upande mwingine ni kwamba anamtazama Shaykh fulani na Shaykh fulani – kama alivosema muulizaji – ni nani ambaye yuko katika njia ya sawasawa na anayefuata mfumo wa Salaf. Huyu ndiye ambaye tunaweka mikono yetu kwenye mkono wake. Sio kwa sababu tuna ushabiki kwake. Isipokuwa ni kwa sababu yuko katika haki na sisi tunaafikiana pamoja naye juu ya haki na vilevile tunapita juu ya njia moja kwa kutendea kazi maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):
وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
“Kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kuwa na uchaji.” ( 06:153)
Ama yule mwenye kuwafanya Mashaykh na viongozi wengine na akaafikiana nao katika yaliyo ya sawa na ya makosa kwa njia ya kwamba hawatoki ndani ya mfumo wao – ni mamoja wamepatia au wamekosea – hawa kwa kweli ndio wale ambao wamezifanyia vibaya nafsi zao na wamewafanyia vibaya wengine vilevile. Wasipotubia basi hawa ndio wana haki zaidi ya kulaumiwa. Jambo liko wazi. Mtu hatakiwi kudangana juu ya jambo lake katika qadhiya hii. Wale wanaopita katika njia [ilionyooka], basi sisi tuko pamoja nao na tunafuata njia moja ambayo Allaah ametuamrisha kwayo na tukalinganiwa nayo na Mtume wetu (´alayhis-Salaam). Achana na wale wanaotengeneza njia katika mambo yao au baadhi ya mambo yao. Kwani hakuna anayefuatwa katika kila kitu isipokuwa tu Mtume wa Allaah. Kuhusu watu wanapatia na wanakosea. Sisi hatuwafuati na wala hatuko nyuma yao kwa sababu tu ni Mashaykh, walinganizi au viongozi. Wewe kuwa pamoja na watu wanaofuata mfumo wa Salaf ambao wanafuata mfumo na ufahamu sahihi.
- Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=163317
- Imechapishwa: 01/09/2018

Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=163317
Imechapishwa: 01/09/2018
https://firqatunnajia.com/ushabiki-ni-kwa-mtume-pekee-na-si-kwa-mashaykh-na-maimamu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)