Swali: Je, Hadiyth isemayo:
“Hakuna usengenyi kwa fasiki”
ni Swahiyh?
Jibu: Si Swahiyh. Lakini zimekuja dalili zinazoonyesha kuwa inajuzu kumsema mtu fasiki kwa yale aliyoyadhihirisha. Mfano ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomruhusu kuingia kwake mtu fulani, akasema:
“Ni mbaya ndugu wa kabila!”
au:
“Ni mbaya mtoto wa kabila!”
Alipoingia alimkaribisha, basi ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) akamuuliza kuhusu hilo, akasema: “Ee ´Aaishah! Hakika watu wabaya zaidi ni wale ambao watu wanawaacha kwa kuogopa shari yao.”
Makusudio ni kwamba ikiwa mtu anajulikana kwa Bid´ah au kwa ufasiki ulio wazi, basi hana usengenyi katika hilo alilolidhihirisha. Akisemwa huyu fulani anafanya hivi, jihadharini naye, jiepusheni naye, basi hilo si usengenyi kwa upande wa jambo alilolidhihirisha la Bid´ah na maovu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3356/درجة-حديث-لا-غيبة-في-فاسق
- Imechapishwa: 15/08/2026
Swali: Je, Hadiyth isemayo:
“Hakuna usengenyi kwa fasiki”
ni Swahiyh?
Jibu: Si Swahiyh. Lakini zimekuja dalili zinazoonyesha kuwa inajuzu kumsema mtu fasiki kwa yale aliyoyadhihirisha. Mfano ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomruhusu kuingia kwake mtu fulani, akasema:
“Ni mbaya ndugu wa kabila!”
au:
“Ni mbaya mtoto wa kabila!”
Alipoingia alimkaribisha, basi ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) akamuuliza kuhusu hilo, akasema: “Ee ´Aaishah! Hakika watu wabaya zaidi ni wale ambao watu wanawaacha kwa kuogopa shari yao.”
Makusudio ni kwamba ikiwa mtu anajulikana kwa Bid´ah au kwa ufasiki ulio wazi, basi hana usengenyi katika hilo alilolidhihirisha. Akisemwa huyu fulani anafanya hivi, jihadharini naye, jiepusheni naye, basi hilo si usengenyi kwa upande wa jambo alilolidhihirisha la Bid´ah na maovu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3356/درجة-حديث-لا-غيبة-في-فاسق
Imechapishwa: 15/08/2026
https://firqatunnajia.com/usengenyi-kwa-fasiki/