Swali: Ikiwa mtu anamwona mwingine akifanya jambo linalokwenda kinyume na Shari´ah, naye hamjui, na anaogopa kwamba akimnasihi hatakubali, je, inajuzu kuchelewesha nasaha hiyo mpaka abadilishe kwa vitendo, kwa kutembea naye hadi atambue kosa lake na akubali bila kumwambia au ni lazima amkanye mara tu anapomuona katika kosa?

Jibu: Ikiwa mtu anaona kwa dhahiri kuwa ni muislamu kisha anamuona katika kosa, basi amweleze kwa maneno mazuri na mtindo mzuri na amlinganie kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) wala asicheleweshe. Huenda asimwone tena baada ya hapo, huenda akafa kabla ya hapo. Kwa maana kheri ya wema ni kuifanya haraka. Kuamrisha mema na kukataza maovu ni jambo lililowekwa, halicheleweshwi isipokuwa ikiwa anaona kwamba hatakubali kwake na tayari amemjaribu. Katika hali hiyo, anapaswa kwenda kwake akiwa na watu wawili au watatu miongoni mwa watu wake wema anaowajua ili hilo liwe lenye kukubalika zaidi katika ulingano na karibu zaidi kuathiri. Ama ikiwa anaogopa kupitwa na fursa, basi anapaswa kukemea maovu kwa mtindo mzuri anaoweza kumshawishi nao, amuombe Mola wake msaada katika hilo na amuombee uongofu. Wala asifanye ukali wala kufanya ukali, bali atumie maneno anayodhani na kutarajia yatafaa katika kumkanya, kama vile kuacha swalah, kujionyesha kwa kunywa vileo, kuwaasi wazazi, kukata uhusiano wa jamaa, kunyoa ndevu, kushusha nguo chini ya vifundo na mengineyo katika maovu yaliyo wazi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3364/كيفية-امر-الشخص-الذي-لا-يعرف-بالمعروف-ونهيه-عن-المنكر
  • Imechapishwa: 15/08/2026