Uoagaji kwa ambaye amelazimishwa kufanya tendo la ndoa bila kumwaga

Swali: Vipi kuhusu aliyelazimishwa kufanya tendo la ndoa?

Jibu: Ni jambo lenye kuhitaji kutazamwa na Allaah anajua zaidi. Ikiwa manii yametoka, basi ataoga kwa ajili ya janaba. Lakini kama amelazimishwa na manii hayakutoka, hapa ndipo mahali panahitaji kutazwa vyema. Huenda kuoga kukawa karibu zaidi na usahihi, kwa sababu linaingia katika maneno (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Pindi tupu mbili zinapogusana… ”

Hivyo huenda hilo likawa karibu zaidi na usahihi. Vivyo hivyo mtu aliyelala kisha akajua kwamba ameingiza tupu yake, inaweza kusemwa kwamba aoge kwa kushika tahadhari, hata kama hakukusudia. Ama kuhusu ulazima, ni jambo lenye kuhitaji kutazamwa vizuri, kwa sababu hakuwa na kusudi wala hakufanya kwa kutaka kwake mwenyewe.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31526/هل-يجب-الغسل-على-من-اكره-على-الجماع
  • Imechapishwa: 31/10/2025