Ibn Baaz kuhusu Hadiyth ya kutochenguka wudhuu´ kwa aliyegusa tupu yake

Swali: Vipi kuhusu Hadiyth isemayo:

“Hakika si vyenginevyo hiyo [tupu yako] ni kipande chako wewe mwenyewe.”?

Jibu: Ni Hadiyth dhaifu. Wengine wamesema imefutwa, na wengine wamesema ni yenye kupingana na iliyo Swahiyh. Katika cheni yake kuna maneno ya kuzungumzwa. Lakini jibu bora zaidi ni kwamba ni Hadiyth yenye kupingana na iliyo Swahiy au imefutwa.

Swali: Vipi kuhusu ambao wamesema kuwa inafanyiwa kazi?

Jibu: Hapana, hilo ni kosa. Hadiyth Swahiyh zipo nyingi kuhusu wajibu wa wudhuu´.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31524/ما-صحة-حديث-انما-هو-بضعة-منك
  • Imechapishwa: 31/10/2025