Swali: Unyenyekevu unakuwa ndani ya moyo?

Jibu: Na kwenye viungo vya mwili pia:

قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ

“Hakika wamefaulu waumini; ambao katika swalah zao ni wenye kunyenyekea.”[1]]

Chimbuko na unyenyekevu ni moyoni. Moyo ukinyenyekea viungo pia vitanyenyekea. Isitoshe utulivu ni nguzo miongoni mwa nguzo za swalah ambayo ni lazima itekelezwe.

[1] 23:01-02

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23750/هل-الخشوع-يكون-في-القلب-والجوارح
  • Imechapishwa: 20/04/2024