Swali: Kufa kwa watoto ni miongoni mwa sababu za kusamehewa madhambi ya mtu?

Jibu: Yote haya yamening´inizwa; miongoni mwayo ni sababu za kuingia Peponi, kuharamishiwa Moto, kuwafikishwa kutenda matendo mema, kusamehewa makosa na mkusanyiko wa mambo hayo.

Swali: Matendo yao yatapitishwa juu ya daraja?

Jibu: Ndio, ni mtihani. Mtihani huleta matokeo mengi. Unaweza kupelekea Allaah akamuwafikisha mja kutenda matendo mema na matukufu kwa sababu ya subira, kutaraji kwake malipo, utakasifu wake wa imani na kadhalika. Aidha inaweza kumpelekea pia kusamehewa makosa, kwa sababu ni miongoni mwa sababu za kusamehewa na kufutiwa makosa. Inaweza kupelekea katika yote mawili; Allaah kumuwafikisha kutenda mema na kufutiwa makosa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23960/هل-موت-الاطفال-من-اسباب-دخول-الجنة
  • Imechapishwa: 03/08/2024