Swali: Miongoni mwa maneno ya Ibn Mas´uud amesema kuwa nyimbo na muziki vinapelekea katika ukafiri?

Jibu: Anachokusudia ni kwamba ni njia inayopelekea huko. Ni kama ilivyo katika upokezi wa Ibn Mas´uud:

“Nyimbo inazalisha unafiki ndani ya moyo.”[1]

Maasi ni posta ya ukafiri kama ambavo maradhi ni posta ya kifo. Maasi yanaweza kumvuta mtu kwenda katika ukafiri. Miongoni mwayo ni nyimbo na ukafiri. Vinaweza kumvuta mtu kidogo kidogo mpaka vikamwingiza ndani ya ukafiri.

[1] Abu Daawuud (4927). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (4927).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat ´alaal-Fatwaa al-Hamawiyyah al-Kubraa, uk. 170-171
  • Imechapishwa: 14/02/2023