´Umrah imefanywa ndani ya Ramadhaan?

Swali: Kuna mtu ameingia katika ´Umrah na akaleta Talbiyah adhuhuri ya tarehe 30 Ramadhaan. Akafika Makkah alfajiri ya siku ya ´iyd na akatimiza ´Umrah yake baada ya swalah ya ´iyd. Je, ´Umrah yake inahesabiwa ameifanya ndani ya Ramadhaan?

Jibu: Kinachozingatiwa ni ule wakati wa Ihraam. Inazingatiwa imefanywa ndani ya Ramadhaan. Muda wa kuwa amefanya Ihraam ndani ya Ramadhaan basi ni ´Umrah iliyofanywa ndani ya Ramadhaan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22996/حكم-من-احرم-اخر-رمضان-واتم-عمرته-بعده
  • Imechapishwa: 07/10/2023