Swali: Muda wa kupangusa kwa mkazi ni mchana mmoja na usiku wake. Ni ipi hukumu ikiwa muda umeisha nami niko safarini umbali wa takriban kilomita 200? Je, niendelee na kuswali au nisubiri mpaka nifike mji ninaoeshi?

Jibu: Ikiwa muda umeisha, inatosha kufanya Tayammum endapo huna maji. Ikiwa muda wa kupaka umeisha na huna maji, hakuna haja ya kuzivua. Unaenda kwenye udongo na unafanya Tayammum. Hapo ni pale uko jangwani na huna maji. Ama ikiwa uko na maji, basi zivue baada ya muda kukamilika, utawadhe na uoshe miguu yako. Ikiwa uko safarini na huna maji, basi maoni sahihi kwa mujibu wa wanazuoni ni kwamba hakuna haja ya kuzivua kwa sababu kutovizua. Kupaka ni kwa uso na viganja tu na wala hakuna haja ya kuzivua.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1937/حكم-من-انتهت-مدة-مسحه-على-الخفين-ولم-يجد-ماء
  • Imechapishwa: 04/07/2026