Swali: Nilitekeleza faradhi ya Hajj mwaka uliopita na nilipomaliza matendo ya Hajj nilienda Tan‘iym, nikahirimia ´Umrah, nikaingia ndani ya Haram, nikatekeleza matendo ya ´Umrah ya Twawaaf, Sa‘y na kunyoa. Kisha nikaondoka wakati huohuo kutoka Makkah al-Mukarramah bila kufanya Twawaaf ya kuaga kwa ujinga wangu, kwa sababu nilidhani kuwa Twawaaf ya ´Umrah inanitosha. Ni ipi hukumu?
Jibu: Inatosha. Maadamu ulifanya Twawaaf, ukafanya Sa‘y na ukaondoka mara moja, inatosha. Twawaaf ya ´Umrah inatosha, kama ilivyokuja katika Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwamba alifanya Twawaaf kwa ajili ya ´Umrah yake kisha akaondoka pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wala haikutajwa kwamba alifanya Twawaaf baada ya Twawaaf ya ´Umrah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1934/حكم-من-حج-ثم-اعتمر-ثم-سافر-ولم-يطف-طواف-الوداع
- Imechapishwa: 04/07/2026
Swali: Nilitekeleza faradhi ya Hajj mwaka uliopita na nilipomaliza matendo ya Hajj nilienda Tan‘iym, nikahirimia ´Umrah, nikaingia ndani ya Haram, nikatekeleza matendo ya ´Umrah ya Twawaaf, Sa‘y na kunyoa. Kisha nikaondoka wakati huohuo kutoka Makkah al-Mukarramah bila kufanya Twawaaf ya kuaga kwa ujinga wangu, kwa sababu nilidhani kuwa Twawaaf ya ´Umrah inanitosha. Ni ipi hukumu?
Jibu: Inatosha. Maadamu ulifanya Twawaaf, ukafanya Sa‘y na ukaondoka mara moja, inatosha. Twawaaf ya ´Umrah inatosha, kama ilivyokuja katika Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwamba alifanya Twawaaf kwa ajili ya ´Umrah yake kisha akaondoka pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wala haikutajwa kwamba alifanya Twawaaf baada ya Twawaaf ya ´Umrah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1934/حكم-من-حج-ثم-اعتمر-ثم-سافر-ولم-يطف-طواف-الوداع
Imechapishwa: 04/07/2026
https://firqatunnajia.com/ameacha-twawaaf-ya-kuaga-kwa-sababu-ya-ujinga/