Swali: Ikibainika baada ya ndoa kuwa mmoja wa wanandoa ana kasoro au upungufu wa kijinsia. Ni ipi fidia kwa mwenzi mwingine katika hali hii?
Jibu: Iwapo mume atabainika kuwa na kasoro au mke akabainika kuwa na kasoro, basi wakikubaliana wao kwa wao na kufanya suluhu ni vyema. Vinginevyo mahakama ndiyo itakayohukumu kati yao. Suala hili linahitaji ufafanuzi. Iwapo mwanamke atamkuta mume wake ana kasoro, kama ugonjwa wa ndani unaoathiri, kushindwa kutekeleza tendo la ndoa au mfano wa kasoro kama hizo, au mume akamkuta mke wake ndiye mwenye kasoro, kama ugonjwa wa ndani au maradhi yanayomfanya awe na kasoro, basi wakipatana wao kwa wao na kila mmoja akamridhia mwenzake au mume akamuacha kwa kutaka kwake mwenyewe au mke akatoa fidia fulani kisha wakaachana, basi ni sawa na jambo hilo linakuwa limekwisha. Ama ikiwa hali hiyo itasababisha ugomvi na mfarakano, basi hukumu yake hurejeshwa kwa mahakama.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2117/حكم-فسخ-عقد-الزواج-لوجود-العيب
- Imechapishwa: 04/07/2026
Swali: Ikibainika baada ya ndoa kuwa mmoja wa wanandoa ana kasoro au upungufu wa kijinsia. Ni ipi fidia kwa mwenzi mwingine katika hali hii?
Jibu: Iwapo mume atabainika kuwa na kasoro au mke akabainika kuwa na kasoro, basi wakikubaliana wao kwa wao na kufanya suluhu ni vyema. Vinginevyo mahakama ndiyo itakayohukumu kati yao. Suala hili linahitaji ufafanuzi. Iwapo mwanamke atamkuta mume wake ana kasoro, kama ugonjwa wa ndani unaoathiri, kushindwa kutekeleza tendo la ndoa au mfano wa kasoro kama hizo, au mume akamkuta mke wake ndiye mwenye kasoro, kama ugonjwa wa ndani au maradhi yanayomfanya awe na kasoro, basi wakipatana wao kwa wao na kila mmoja akamridhia mwenzake au mume akamuacha kwa kutaka kwake mwenyewe au mke akatoa fidia fulani kisha wakaachana, basi ni sawa na jambo hilo linakuwa limekwisha. Ama ikiwa hali hiyo itasababisha ugomvi na mfarakano, basi hukumu yake hurejeshwa kwa mahakama.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2117/حكم-فسخ-عقد-الزواج-لوجود-العيب
Imechapishwa: 04/07/2026
https://firqatunnajia.com/mmoja-wa-wanandoa-amemkuta-mwenzie-ana-kasoro-au-upungufu/