Swali: Katika maisha yangu nimekumbana na matatizo mengi jambo ambalo limenifanya kuyachukia maisha. Kila wakati ninapokuwa vibaya basi humwelekea Allaah na kumwomba anifishe haraka iwezekanavyo. Mpaka hii leo nahisi hivo, kwa sababu sioni kingine ambacho ni suluhu ya matatizo yangu zaidi ya kifo. Je, napata dhambi?
Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Asitamani yeyote kifo kutokana na dhara lililompata. Ikiwa hana budi isipokuwa kufanya hivo, basi na aseme:
اللهُمَّ أَحْيِنِي مَا كَانَتِ الْحَيَاةُ خَيْرًا لِي، وَتَوَفَّنِي إِذَا كَانَتِ الْوَفَاةُ خَيْرًا لِي
“Ee Allaah! Nipe uhai muda wa kuwa uhai ni kheri kwangu. Na nifishe ikiwa kifo ni kheri kwangu.”[1]
Kwa hiyo haifai kwa yeyote aliyepatwa na janga, dhiki au shida kutamani kifo. Bali ni lazima kwake kusubiri na kutaraji malipo kutoka kwa Allaah na asubiri faraja kutoka Kwake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Tambua ya kwamba nusura iko pamoja na subira, faraja iko pamoja na dhiki, uzito uko pamoja na wepesi.”[2]
Aidha atambue yule aliyepatwa na msiba wowote ya kwamba matatizo yanayompata ni kifutio cha madhambi yake yaliyotangulia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna muislamu anayefikwa na machovu, tabu, ugonjwa, hamu, huzuni mpaka mwiba ukimchoma, isipokuwa Allaah anamfutia makosa yake.”[3]
Pamoja na kusubiri na kutaraji malipo kutoka kwa Allaah mtu anafikia ngazi ya wale wenye kufanya subira. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu wenye kufanya subira:
وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ
”Bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu kidogo katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao [ya kazi zenu]. Wabashirie wenye kusubiri ambao unapowafika msiba basi husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.”[4]
Kwa hiyo naona kuwa mtazamo wa mwanamke huyu ni wa makosa pale anapoona kuwa kifo ndio ufumbuzi pekee. Kifo hakimalizi matatizo yake. Pengine mambo yakawa mabaya zaidi baada ya yeye kufa. Kuna watu wengi wanaoptwa na majanga na bado wanaendelea kutenda madhambi; hawaachi kuendelea kutenda dhambi na wala hawatubii kwa Allaah. Pindi watu kama hawa wanapokufa wanajiharakishia tu kuadhibiwa. Ingelikuwa ni vyema kwao kama wangeendelea kuishi, wakatubia kwa Allaah (Ta´ala), wakamuomba Allaah msamaha, wakasubiri matatizo na kusubiri faraja. Kwa hivyo ni juu yako, ee dada, kusubiri na kutaraji malipo kutoka kwa Allaah na kusubiri faraja kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) ambaye amesema:
فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا
“Hakika pamoja na kila gumu kuna wepesi. Hakika pamoja na kila ugumu kuna wepesi!”[5]
Vilevile imesihi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Tambua ya kwamba nusura iko pamoja na subira, faraja iko pamoja na dhiki, uzito uko pamoja na wepesi.”
[1] al-Bukhaariy (5671) na Muslim (2680).
[2] Ahmad (1/307).
[3] al-Bukhaariy (5641-5642).
[4] 2:155-156
[5] 94:5-6
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/60-62)
- Imechapishwa: 30/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/60-62)
Imechapishwa: 30/07/2026
https://firqatunnajia.com/umechoka-na-maisha/