113 – Inapendekezwa kupapasa kichwa cha yatima na kumkirimu. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya ´Abdullaah bin Ja´far aliyesema:
“Kama ungekuwa umeniona mimi, Qutham na ´Ubaydullaah bin ´Abbaas tulipokuwa watoto tukicheza. Tahamaki Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipita akiwa juu ya mnyama wake ambapo akasema: ”Muinueni huyu kwangu!”, akaniweka mbele yake. Akasema: ”Muinueni huyu kwangu!”, akaniweka nyuma yake. ´Ubaydullaah alikuwa mpendwa zaidi kwa ´Abbaas kuliko Qutham, lakini hakupata haya mbele ya ami yake kwa kumchukua Qutham na kumuacha yeye. Kisha alipapasa kichwa changu mara tatu. Kila alipompapasa alisema:
اللهم اخلف جعفرا في ولده
”Ee Allaah, mpe mrithi Ja´far katika watoto wake.”
Nikamuuliza ´Abdullaah: ”Qutham alipata nini?” Akasema: ”Alifariki hali ya kuwa shahidi.” Nikasema: ”Allaah na Mtume Wake wanajua zaidi kuhusu kheri.” Akasema: ”Ndio.”
Ameipokea Ahmad (1760) ambaye tamko ni lake, al-Haakim (1/372), al-Bayhaqiy (4/60) na cheni yake ya wapokezi ni nzuri. al-Haakim amesema: “Swahiyh.”
adh-Dhahabiy ameafikiana naye.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 212
- Imechapishwa: 30/07/2026
113 – Inapendekezwa kupapasa kichwa cha yatima na kumkirimu. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya ´Abdullaah bin Ja´far aliyesema:
“Kama ungekuwa umeniona mimi, Qutham na ´Ubaydullaah bin ´Abbaas tulipokuwa watoto tukicheza. Tahamaki Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipita akiwa juu ya mnyama wake ambapo akasema: ”Muinueni huyu kwangu!”, akaniweka mbele yake. Akasema: ”Muinueni huyu kwangu!”, akaniweka nyuma yake. ´Ubaydullaah alikuwa mpendwa zaidi kwa ´Abbaas kuliko Qutham, lakini hakupata haya mbele ya ami yake kwa kumchukua Qutham na kumuacha yeye. Kisha alipapasa kichwa changu mara tatu. Kila alipompapasa alisema:
اللهم اخلف جعفرا في ولده
”Ee Allaah, mpe mrithi Ja´far katika watoto wake.”
Nikamuuliza ´Abdullaah: ”Qutham alipata nini?” Akasema: ”Alifariki hali ya kuwa shahidi.” Nikasema: ”Allaah na Mtume Wake wanajua zaidi kuhusu kheri.” Akasema: ”Ndio.”
Ameipokea Ahmad (1760) ambaye tamko ni lake, al-Haakim (1/372), al-Bayhaqiy (4/60) na cheni yake ya wapokezi ni nzuri. al-Haakim amesema: “Swahiyh.”
adh-Dhahabiy ameafikiana naye.
Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 212
Imechapishwa: 30/07/2026
https://firqatunnajia.com/111-mapendekezo-ya-kupapasa-kichwa-cha-yatima/