112 – Sunnah ni kwamba watu wa karibu na majirani wa maiti ndio waandae chakula kwa ajili ya familia ya maiti ili kuwatosheleza. Hili ni kwa mujibu wa Hadiyth ya ´Abdullaah bin Ja´far (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:
“Wakati ilipokuja khabari ya kifo cha Ja´far Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:
‘Waandalieni familia ya Ja´far chakula, kwani wamejiliwa na jambo linalowashughulisha au wamejiliwa na kinachowashughulisha.’”
Ameipokea Abu Daawuud (2/59), at-Tirmidhiy (2/134) na ameipa daraja ya kuwa nzuri, pia Ibn Maajah (1/490), vilevile ash-Shaafi´iy katika “al-Umm” (1/247), ad-Daaraqutwniy (194, 197), al-Haakim (1/372), al-Bayhaqiy (4/61), Ahmad (1/175). al-Haakim amesema:
“Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.”
adh-Dhahabiy ameafikiana naye. Ibn as-Sakan pia ameisahihisha kama ilivyokuja katika “at-Talkhiysw” (5/253). Nami naona kuwa ni Hadiyth nzuri, kama alivosema at-Tirmidhiy, kwani kuna nyingine inayoipa nguvu kutoka kwa Hadiyth ya Asmaa’ bint ´Umays, jambo ambalo nimelibainisha katika “at-Ta´aliqaat al-Jiyaad”.
[´Aaishah alikuwa akiagiza atayarishiwe talbina kwa ajili ya mgonjwa na mwenye huzuni kwa ajili ya aliyefariki ambapo akisema: “Hakika mimi nimesikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
”Hakika talbina hutuliza moyo[1] wa mgonjwa na huondoa baadhi ya huzuni.’”
Ameipokea al-Bukhaariy (10/119-120) ambaye tamko ni lake, Muslim (7/26), al-Bayhaqiy (4/61) na Ahmad (6/155).]
Imaam ash-Shaafi’iy amesema katika ”al-Umm” (1/247):
“Napendelea majirani wa marehemu au ndugu wa karibu wawe ndio wanaowaandalia familia ya mfiwa chakula siku ya kifo na usiku wake chenye kuwatosheleza. Hakika hiyo ni Sunnah, na ni ukumbusho mzuri. Isitoshe ni moja ya matendo ya watu wema kabla na baada yetu.”
Kisha akataja Hadiyth iliyotajwa hapo juu kutoka kwa ´Abdullaah bin Ja´far.
[1] Talbina ni supu iliyotengenezwa kutoka kwa unga au ngano. Wakati mwingine huchanganywa na asali.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 211-212
- Imechapishwa: 30/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 211-212
Imechapishwa: 30/07/2026
https://firqatunnajia.com/110-jamaa-na-majirani-kuandaa-chakula-kwa-ajili-ya-familia-ya-maiti/