Swali: Baadhi ya wagonjwa wanaacha kuswali kwa hoja ya kwamba hawawezi kutawadha na nguo zao zina najisi. Ni ipi hukumu?
Jibu: Kitendo hichi ni ujinga na ni khatari. Ni wajibu kwa muislamu kuswali kadri na anavyoweza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia ´Imraan bin Huswayn (Radhiya Allaahu ´anh):
“Swali kwa kusimama. Usipoweza, kwa kukaa. Usipoweza, kwa kulalia ubavu.”[1]
Allaah (Ta´ala) amesema:
وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ
”Mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu akitoka chooni au mmewagusa wanawake, kisha hamkupata maji, basi fanyeni Tayammum kwa ardhi ilio safi panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu.”[2]
Allaah amemfanya mgonjwa ambaye hawezi kuyatumia maji badala yake kufanya Tayammum.
Vivyo hivyo inapokuja katika swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amejaalia hatua mbalimbali kutegemea na uwezo wa mtu na akasema:
“Swali kwa kusimama. Usipoweza, kwa kukaa. Usipoweza, kwa kulalia ubavu.”
Kwa hiyo kimsingi ni kwamba ni wajibu kwa mgonjwa kutawadha. Asipoweza atafanya Tayammum. Baada ya hapo ataswali kwa kusimama. Asipoweza basi ataswali kwa kuketi chini na ataashiria wakati wa Rukuu´ na Sujuud ambapo atainama chini zaidi Sujuud kuliko katika Rukuu´. Hapo ni pale ambapo hawezi kusujudu. Akiweza kusujudu basi atafanya hivo. Asipoweza kuketi chini basi ataswali kwa kulalia ubavu na kuashiria wakati wa kurukuu na kusujudu. Asipoweza kutikisika kabisa lakini bado yuko na fahamu timamu, atanuia kuswali na matendo yake kimoyoni. Atachoweza kusoma atakisoma, ikiwa ni pamoja na al-Faatihah. Wakati anapofika katika Rukuu´, basi atanuia Rukuu´, na kusema:
الله أكبر
“Allaah ni mkubwa.”
na:
سبحان ربي العظيم
“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”
Kisha atasema:
سَمعَ الله لِمنْ حَمِدَه
“Allaah amemsikia mwenye kumuhimidi.”
Halafu atanuia kuinuka na namna hiyo matendo mengine. Haijuzu kwake kuchelewesha swalah nje ya wakati wake. Hata kama tutakadiria kuwa yuko na najisi katika mwili, nguo au godoro lililo chini yake na asiweze kuliondosha, basi analazimika kuswali kwa kiasi cha atachoweza, kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[3]
[1] al-Bukhaariy (1117).
[2] 5:6
[3] 64:16
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/96-97)
- Imechapishwa: 30/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/96-97)
Imechapishwa: 30/07/2026
https://firqatunnajia.com/mgonjwa-anaacha-kuswali/