Swali: Vipi tutaoanisha baina ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Kila Bid´ah ni upotevu.”
na maneno ya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh):
“Neema ya Bid´ah iliyoje hii.”?
Jibu: Ni kipi anacholenga ´Umar? Analenga swalah ya Tarawiy nyuma ya imamu. Tarawiyh ni Sunnah na sio Bid´ah. Anachomaanisha ni Bid´ah ya kilugha. Kwa sababu ni kitu ambacho watu walikisahau ambapo ´Umar akawa amekihuisha na kusema:
“Neema ya Bid´ah iliyoje hii.”
Anamaanisha Bid´ah kilugha na sio Kishari´ah. Bid´ah za Kishari´ah zote ni batili:
“Kila Bid´ah ni upotevu.”
Haiwezekani kabisa ikawa ´Umar anamaanisha Bid´ah ya Kishari´ah. Tarawiyh sio Bid´ah; bali ni Sunnah. Kuwakusanya wote nyuma ya imamu mmoja sio Bid´ah. Walikuwa wakiswali hivyo nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aliswali nao nyusiku kadhaa. Pindi alipochelea Tarawiyh isije kufaradhishwa juu yao ndipo akawa ameacha. Wakati wa ´Umar khofu ikawa imeondoka kwa kuwa imeisha kwa kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakufaradhishwi kitu baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakati khatari ilipotoweka ndipo ´Umar akawakusanya na akaihuisha Sunnah ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiitendea kazi na akawa ameaiacha kwa kuchelea isije kufaradhishwa.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–14330804.mp3
- Imechapishwa: 09/06/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)