Swali: Ni Sunnah kufunika kichwa wakati wa swalah?

Jibu: Ndio. Kujipamba katika swalah ni jambo linalotakikana:

يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ

“Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu wakati wa kila swalah.” (07:31)

Mapambo ni kufunika viungo vya siri na ni kujipamba kwa wasaa, kama alivyosema Shaykh-ul-Islaam. Umesimama mbele ya Mola Wako. Hivyo unatakiwa uwe katika muonekano mzuri kadri na inavyowezekana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–14330804.mp3
  • Imechapishwa: 09/06/2020