Mume anakuja mbele ya masomo na kazi

Swali: Ni kipi kinachoniwajibikia ikiwa mwanaume mwema atamchumbia mwanamke ambaye mimi ndiye msimamizi wake na nikawa nimemkatalia ili aweze kutimiza masomo yake au apate kazi?

Jibu: Kinachokuwajibikia ni wewe kutubu kwa Allaah. Akija mwanaume mwema kumchumbia muozeshe. Usimpoteze. Usimpotezee manufaa yake. Masomo sio jambo la lazima. Kazi sio jambo la lazima. Muhimu ni mwanamke aweze kupata mwanaume mwema. Ukipata mwanaume kama huyo usimzembee.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–14330804.mp3
  • Imechapishwa: 09/06/2020