Swali: Ikiwa upande mmoja wa kulia kuna kundi linalolingania kwa Allaah na upande wa pili kuna kundi lingine linalolingania kwa Allaah. Hata hivyo kundi la upande wa kulia linalitukana hilo lingine la kushoto na kinyume chake. Katika hali hiyo mtu afanye nini?

Jibu: Kilicho cha wajibu ni kuwanasihi ili wawe kitu kimoja na kuwatahadharisha kutokamana na mfarakano ili wafahamiane na kuondoke matatizo. Ama kitendo cha kugongana kinawakimbiza watu kutokamana na ulinganizi. Kitendo hicho kinawafanya wajinga kujiuliza haki iko na nani. Hii ni fitina. Ni lazima kukusanyika, kusaidiana na kuondosha tofauti kwa njia zinazokubalika katika Shari´ah. Ni lazima kwa wanazuoni na watu wa kheri wawanasihi na kukaa katikati yao ili tofauti imalizike na wawe kitu kimoja katika kulingania.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21534/حكم-الاختلاف-والتفرق-بين-جماعات-الدعوة
  • Imechapishwa: 22/08/2022