Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nyoyo za wanaadamu zote ziko kati ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa huruma, kama vile moyo mmoja; anazigeuza vile Atakavyo.” Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Allaah, ambaye unazigeuza nyoyo! Zigeuze nyoyo zetu katika utiifu Wako.”[1]

Mimi mwenyewe siwezi kujiongoza. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye mwenye kuniongoza na kunifanya imara. Sababu ya hilo ni kwamba kuna kundi la wakuwait walikuja Yemen na wakaniomba kuungana nao. Nikawaambia kama wanataka kusaidia ulinganizi wetu bila ya kuweka vikwazo wala masharti yoyote, basi nitafanya, vinginevyo hapana. Wakawatafuta baadhi ya ndugu zetu wenye tamaa ambao wakawapokea. Mpaka katika kikao kimoja alisema mmoja katika wakuwait hao:

“Ulingano wetu haukupata nguvu isipokuwa baada ya kuwaacha wanazuoni.”

Mmoja wa waliohudhuria mkutano huo alisema kuwa maneno hayo yalimtia baridi, lakini hata leo anayakimbilia. Watu lazima wajue msimamo wetu ya kwamba tunajitenga na Hizbiyyuun wote.

[1] Muslim (2654), Ahmad (2/168) na an-Nasaa’iy (7739).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 120-121
  • Imechapishwa: 16/02/2025