Ulazima wa kuyatolea zakaah mapambo ya wanawake

2978- Faatwimah bint Qays (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Nilimwendea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nikiwa na dhahabu yenye uzito wa 70 ambapo nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Chukua kutoka hapo ile faradhi ambayo Allaah amefaradhisha.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akachukua uzito wa 1.75. Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Chukua kutoka hapo ile faradhi ambayo Allaah amefaradhisha.” Hivyo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaigawa kwa makundi haya masita na wengine kisha akasema: “Ee Faatwimah! Hakika wa haki (´Azza wa Jall) hakukuachia chochote.” Ndipo nikasema: “Nimeridhia kile alichokiridhia Allaah (´Azza wa Jall) na Mtume Wake.”

Ameipokea Abush-Shaykh katika “Intiqaa´ Ibn Marduuyah”. Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.

Katika Hadiyth, kama ilivyo katika Hadiyth zengine zote ambazo ni Swahiyh nilizotaja katika “Aadaab-iz-Zifaaf”, ipo dalili ya wazi ya kwamba ni jambo lililokuwa linatambulika vyema katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ulazima wa kutolea zakaah mapambo ya wanawake. Kwa ajili hiyo ndio maana Faatwimah bint Qays alikuja na mkufu wake kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili achukue zakaah yake. Pengine wakakinaika wale ambao bado wanaendelea kutoa fatwa kuwa mapambo hayahitajii kutolewa zakaah na hivyo wakawa wanawanyima mafukara haki yao kutoka katika mali ya wale matajiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (6/2/1183-1885)
  • Imechapishwa: 06/08/2020