Kwa hivyo ni lazima kuwepo upambanuo na tofauti kati ya yule mwenye kumuabudu Allaah kwa kumuamini kwa haki na ukweli, dhahiri na kwa ndani ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah na hayakuumbwa. Ni lazima kuwepo tofauti ya wazi. Tofauti na upambanuo huu hauwezi kupatikana isipokuwa kwa yule mpwekeshaji na mwenye kumuabudu Allaah kumtakasia nia baada ya kusema “Qur-aan ni maneno ya Allaah” aongezee juu yake “Haikuumbwa”. Kwa sababu kwa kufanya hivo ndio kunapambanuka kati ya watu wa uongofu na wapotevu. Na upambanuo huu ni lazima upatikane. Kwa sababu Jahmiy khabithi anasema na yeye kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah, lakini wakati huo huo ameficha fikira zake za [kusema] kwamba maneno ya Allaah – akikusudia Qur-aan hii – yameumbwa. Kwa sababu watu hawa ni wenye kujulikana kwa vitimbi na utatizi na hila. Ni lazima kufunga vizuizi vitakavowafikisha kati yao na yale wanayotaka kuyafikia na kuwazuia na hila hizi. Watazuiwa vipi? Kwa mtu Sunniy kusema hali ya kuwa ni mkweli “Qur-aan haikuumbwa”. Kwa kufanya hivi mtu anakuwa amewafungia njia.
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/403)
- Imechapishwa: 20/05/2015
Kwa hivyo ni lazima kuwepo upambanuo na tofauti kati ya yule mwenye kumuabudu Allaah kwa kumuamini kwa haki na ukweli, dhahiri na kwa ndani ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah na hayakuumbwa. Ni lazima kuwepo tofauti ya wazi. Tofauti na upambanuo huu hauwezi kupatikana isipokuwa kwa yule mpwekeshaji na mwenye kumuabudu Allaah kumtakasia nia baada ya kusema “Qur-aan ni maneno ya Allaah” aongezee juu yake “Haikuumbwa”. Kwa sababu kwa kufanya hivo ndio kunapambanuka kati ya watu wa uongofu na wapotevu. Na upambanuo huu ni lazima upatikane. Kwa sababu Jahmiy khabithi anasema na yeye kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah, lakini wakati huo huo ameficha fikira zake za [kusema] kwamba maneno ya Allaah – akikusudia Qur-aan hii – yameumbwa. Kwa sababu watu hawa ni wenye kujulikana kwa vitimbi na utatizi na hila. Ni lazima kufunga vizuizi vitakavowafikisha kati yao na yale wanayotaka kuyafikia na kuwazuia na hila hizi. Watazuiwa vipi? Kwa mtu Sunniy kusema hali ya kuwa ni mkweli “Qur-aan haikuumbwa”. Kwa kufanya hivi mtu anakuwa amewafungia njia.
Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/403)
Imechapishwa: 20/05/2015
https://firqatunnajia.com/ulazima-wa-kuongeza-sentesi-haikuumbwa__trashed/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)