Swali: Kuhusiana na tofauti juu ya kwamba ni kipi kilichotangulia; ´Arshi au kalamu, vipi mtu ajibu kwa mwenye kusema kuwa Salaf walitofautiana katika mambo ya msingi ikiwa ni pamoja na masuala haya?

Jibu: Haya hayadhuru. Kuna yeyote katika wao aliyepinga ´Arshi? Ikiwa kuna yeyote anayepinga ´Arshi au kalamu hukumu yake inakuwa ipi? [Kufuru].

Haya mengine yanayuhusiana na mambo ya kihistoria kutokana na kila mmoja anavyoyafahamu maandiko juu ya kuwa ni kipi kilichoanza kutangulia. Ama kuhusu ´Arshi ni msingi. Kuamini ´Arshi ndio msingi. Kadhalika kuamini kalamu ndio asli. Mmoja wao akipinga kimoja katika hayo, tunasema kuwa Salaf walitofautiana? Badala yake anafanyiwa Takfiyr na hatusemi kuwa Salaf walitofautiana. Huyu mpingaji hawi Salafiy. Mmefahamu?

Jambo hili halidhuru. Tofauti hii sio katika jambo la msingi, ni katika jambo linaloitwa la kihistoria…

Watu hawa wanatatiza. Salaf hawakutofautiana katika mambo ya msingi. Watu hawa ni watatizi. Kwa nini? Wanachotaka ni sisi kunyamazia tofauti za Raafidhwah, Jahmiyyah, Mu´tazilah na kadhalika kwa madai ya kwamba Salaf pia walitofautiana katika mambo ya msingi. Haya ni katika utatizi na vitimbi ili wampeleke Salafiy katika Hizbiyyah Mumayiy´ ambayo imeupoteza Uislamu, haki na Manhaj ya Salaf.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26882
  • Imechapishwa: 20/05/2015