Swali: Je, kichwa cha al-Husayn bin ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) kiko Misri au kiko ´Iraaq pamoja na mwili wake? Ni ipi hukumu ya kutembelea makaburi yanayodaiwa kuwa ya bibi Zaynab, al-Husayn na wengineo kwa wanaume?
Jibu: Wanazuoni wahakiki wanaona kuwa kile kilichopo Misri hakina msingi wa kweli; si kichwa wala si chochote kinachohusiana na al-Husayn (Radhiya Allaahu ´anh). Hakuna kaburi lake Misri kwa uhakika. al-Husayn (Radhiya Allaahu ´anh) alizikwa katika ardhi ya ´Iraaq. Ama kichwa chake, imepokelewa kuwa kilikuwa katika Shaam wakati wa Yaziyd – na Allaah ndiye Mjuzi zaidi.
Tunachotaka kusema ni kwamba madai ya kuwepo kwake Misri hayana msingi sahihi.
Kuhusu yale makaburi yanayotukuzwa sana katika baadhi ya nchi – kama yanayodaiwa kuwa ya al-Husayn, al-Badawiy, bibi Zaynab, bibi Nafiysah au wengineo – yamesababisha shari kubwa kwa watu wengi kutokana na kupita mipaka katika kuyatukuza. Watu wamefikia kuyaomba, kuyaomba msaada na kuomba uokozi badala ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), jambo ambalo linaingia katika shirki kubwa.
Kwa hiyo ni wajibu kwa wanazuoni wa Misri wote – ninamaanisha wanazuoni wa Sunnah, wanazuoni wa haki – wamche Allaah, wajitayarishe kwa juhudi kubwa na kwa kutarajia yaliyoko kwa Allaah mpaka wawabainishie watu, wawabainishie watu wa kawaida kuhusu shirki hii kubwa inayofanywa katika makaburi, katika kuyazunguka, kuyaomba na kuomba msaada kutoka kwayo. Kwa hakika tumefikiwa na khabari kwa wingi kwamba hata dereva wa teksi anapopita husimama kwenye kaburi akisema “msaada”, kisha anaondoka. Haya ni katika yale yaliyotufikia na yakawa mashuhuri kwetu. Ninachotaka kusema ni kwamba haya ni majanga makubwa yaliyotokea Misri, Shaam, Jordan, ´Iraaq na katika nchi nyingi.
Basi ni wajibu juu ya wanazuoni wachangamke kwa juhudi kubwa sana katika kuwazuia watu wa kawaida na shari hii, kuwabainishia dini kwa kuandika katika magazeti, kuandika katika vitabu vidogo vinavyoenea miongoni mwao, katika Khutbah za ijumaa, Khutbah zinazokuwa katika matukio mbalimbali na katika misikiti ili jambo hili liwe kwa wingi miongoni mwao, ili asiyejua ajifunze na wengine wafundishane wao kwa wao na waeneze maneno haya na nasaha hizi miongoni mwao.
Vivyo hivyo kwa kurekodi na zirekodiwe kanda zisambazwe miongoni mwao ili hilo liongezeke kwao na ili waache batili hii kubwa na shirki mbay. Tunajilinda kwa Allaah, tunamuomba Allaah awaongoze watu wa kawaida na awape wanazuoni tawfiyq ya kutekeleza wajibu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3153/حقيقة-وجود-راس-الحسين-بن-علي-في-مصر
- Imechapishwa: 03/08/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3153/حقيقة-وجود-راس-الحسين-بن-علي-في-مصر
Imechapishwa: 03/08/2026
https://firqatunnajia.com/ukweli-kuhusu-kichwa-cha-al-husan-bin-aliy/