Swali: Kusafiri kwa mwanamke bila Mahram ni haramu, lakini maana ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth inayosema “Safari ya siku moja na usiku mmoja” ni ipi? Je, kusafiri kwa ndege kutoka nchi moja hadi nyingine kwa muda wa saa moja na nusu tu kunahesabika kuwa ni safari iliyo chini ya siku moja na usiku mmoja?
Jibu: Kila kinachoitwa ”safari” kinakatazwa kwa mwanamke isipokuwa awe pamoja na Mahram wake. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanamke asisafiri isipokuwa pamoja na Mahram.”
Hivi ndivyo ilivyokuja katika Hadiyth Swahiyh ndani al-Bukhaariy na Muslim kutokana na riwaya ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa).
Ama yale yaliyokuja katika baadhi ya riwaya ”Siku tatu”, ”Siku moja na usiku mmoja”, ”Siku moja”, ”Usiku mmoja”, au ”Umbali fulani”, wanazuoni wamejibu kwamba hayo yanatofautiana kulingana na maswali yaliyoulizwa. Huyu aliuliza kuhusu siku moja, mwingine kuhusu umbali fulani, mwingine kuhusu siku moja na usiku mmoja, mwingine kuhusu siku mbili na hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akijibu kulingana na swali lililoulizwa, si kwa maana ya kuweka mipaka maalum. Kwa hiyo haikusudiwi kuwekewa mpaka maalum, ndiyo maana riwaya zimekuja kwa namna mbalimbali. Nyingine siku tatu, nyingine siku mbili, nyingine siku moja na usiku mmoja, nyingine usiku mmoja, nyingine siku moja na nyingine umbali fulani. Kigezo ni kile kinachoitwa safari. Kila kinachoitwa safari – ni mamoja iwe ni kwa ndege, treni, gari au ngamia – basi hairuhusiwi kwa mwanamke kusafiri isipokuwa awe na Mahram wake.
Swali: Kuna mfanyakazi hapa amemtuma mke wake kutoka nchi nyingine aje kwake, lakini yeye hawezi kwenda kumchukua?
Jibu: Hili lote ni kosa, yote ni makosa. Ni lazima aende mwenyewe kumchukua au aje ndugu yake kama kaka yake, ami yake au mfano wa hao. Ama yeye kusafiri kwa ndege peke yake, huenda akapatikana mtu wa kumpotosha ndani ya ndege, kumvutia, kuzungumza naye na kumuwekea miadi ya maovu. Pia huenda asimpate Mahram wa kumpokea anapofika uwanjani kutokana na dharurah fulani. Vilevile huenda kukatokea tatizo ndani ya ndege likamlazimu kurudi au kuelekezwa nchi nyingine.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3182/ضابط-السفر-للمراة
- Imechapishwa: 03/08/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3182/ضابط-السفر-للمراة
Imechapishwa: 03/08/2026
https://firqatunnajia.com/kila-inayoitwa-safari/