”Ukitia mafuta kiwango fulani tunakuoshea gari bure”

Swali: Kuna baadhi ya vituo vya mafuta vinavyotoa huduma ya kuosha gari bila malipo kwa mtu yeyote anayenunua gesi kwa pesa 120. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ni bora kuacha kufanya hivo, kwa sababu kufanya hivo ni kuwahamasisha watu wawakimbilie ili wengine waachwe. Bora na vyema zaidi ni kuacha kufanya hivo.

Swali: Je, wakewe ikiwa watafanya hivo?

Jibu: Bora ni kuacha kufanya hivo. Hivo ndio salama zaidi kwangu, kwa sababu anaweza kujitolea pesa kwa matumaini ya kufanikisha hili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23305/حكم-عرض-المحطات-غسيل-السيارة-مجانا
  • Imechapishwa: 31/05/2025