Swali: Mke wangu alikwenda kumtembelea dada yake bila ruhusa yangu ambapo nikakasirika nikamwambia ”Ukikwenda bila ruhusa yangu, basi umeachika, umeachika, umeachika.” Baada ya muda akaenda pamoja na familia yake wakati mimi sipo. Je, talaka inatokea? Sasa nataka kujitoa katika hilo, je, ninawajibika kutoa kafara au nifanye nini?
Jibu: Jambo hili linatofautiana kulingana na nia yako. Ikiwa ulisema maneno hayo kwa lengo la kumzuia tu na hukukusudia talaka, bali ulikusudia kumtisha na kumzuilia, basi hilo linahesabika kuwa ni kiapo. Hivyo ikiwa alikwenda bila ruhusa yako, basi juu yako ni kutoa kafara ya kiapo. Ama ikiwa ulikusudia talaka kweli kwa kusema kwako “Umeachika, umeachika, umeachika”, basi talaka tatu zinatokea. Ikiwa alifanya hicho ulichokataza, basi anakuwa ameharamishwa kwako mpaka aolewe na mume mwingine.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3183/حكم-الطلاق-بالثلاث-في-وقت-واحد
- Imechapishwa: 30/07/2026
Swali: Mke wangu alikwenda kumtembelea dada yake bila ruhusa yangu ambapo nikakasirika nikamwambia ”Ukikwenda bila ruhusa yangu, basi umeachika, umeachika, umeachika.” Baada ya muda akaenda pamoja na familia yake wakati mimi sipo. Je, talaka inatokea? Sasa nataka kujitoa katika hilo, je, ninawajibika kutoa kafara au nifanye nini?
Jibu: Jambo hili linatofautiana kulingana na nia yako. Ikiwa ulisema maneno hayo kwa lengo la kumzuia tu na hukukusudia talaka, bali ulikusudia kumtisha na kumzuilia, basi hilo linahesabika kuwa ni kiapo. Hivyo ikiwa alikwenda bila ruhusa yako, basi juu yako ni kutoa kafara ya kiapo. Ama ikiwa ulikusudia talaka kweli kwa kusema kwako “Umeachika, umeachika, umeachika”, basi talaka tatu zinatokea. Ikiwa alifanya hicho ulichokataza, basi anakuwa ameharamishwa kwako mpaka aolewe na mume mwingine.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3183/حكم-الطلاق-بالثلاث-في-وقت-واحد
Imechapishwa: 30/07/2026
https://firqatunnajia.com/ukienda-kumtembelea-dada-yako-basi-umeachika/