Swali: Ninaona katika jamii wanawake wa kigeni wakifunua nyuso zao kwa mapambo mazuri. Je, inajuzu kuwalaani kwa kusema: “Mwanamke anatoka akiwa ni mzinifu na anarudi akiwa ni mzinifu”?

Jibu: Hairuhusiwi kwako kumlaani. Bali unatakiwa kumuombea uongofu na ukatae maovu anayofanya, lakini usimlaani na wala usimsaidie shaytwaan dhidi yake. Badala yake mlinganie katika kheri, mkataze maovu na umwambie: “Ee mwanamke, mche Allaah! Jisitiri! Jifunge Hijaab!” na umuombee uongofu. Ikiwa ana mume au mlezi, basi mnasihi yeye pia. Hivyo ndivyo inavyopasa kwa muumini.

Swali: Vipi ikiwa ni mwanamke si muislamu?

Jibu: Hata akiwa si muislamu, anaamrishwa mlezi wake amhifadhi kwa Hijaab katika nchi za Kiislamu na pia huombwa mtawala kulisimamia hilo ili asilidhuru jamii na ili wanawake wa Kiislamu wasimuige.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3178/حكم-لعن-المراة-المتبرجة
  • Imechapishwa: 30/07/2026